Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Bw. Ernest M. Mchanga (wa nne kulia)¬ katika picha ya pamoja na Wajumbe na Waalikwa baada ya Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliojadili Taarifa ya Fedha na Utekelezaji wa Mpango wa Kazi wa Tume kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 uliofanyika tarehe 17 Septemba, 2026 mkoani Morogoro.
Baadhi ya Wajumbe na Waalikwa wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika tarehe 17 Septemba, 2026 mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Bw. Ernest M. Mchanga (aliyeketi katikati) akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliojadili Taarifa ya Fedha na Utekelezaji wa Mpango wa Kazi wa Tume kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 uliofanyika tarehe 17 Septemba, 2026 mkoani Morogoro.
Mjumbe wa Sekretarieti, Bw. Said S. Said (kushoto) kutoka Afisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar na Dkt. Remidius D. Ruhinduka – Kaimu Kamishna, Idara ya Uchambuzi wa Sera kutoka Wizara ya Fedha ya SJMT (kulia) ambaye alialikwa katika kikao hicho, wakifuatilia wasilisho la taarifa katika kikao cha Sekretarieti ya Tume kilichofanyika tarehe 29 Septemba, 2026.
Bw. Francis R. Daggo – Mchumi (wa kwanza kushoto) akiwasilisha Rasimu ya Stadi na Taarifa ya Ziara ya Mafunzo nchini China kuhusu Uhusiano wa Kifedha kati ya Serikali ya Watu wa China na Serikali ya Eneo Maalumu la Utawala la Hong Kong katika kikao cha Sekretarieti ya Tume kilichofanyika tarehe 29 Septemba, 2026.
Kaimu Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Tume ya Pamoja ya Fedha, Dkt. Ephraim O. Mdee (kushoto) na Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha, Bw. Ernest M. Mchanga wakifuatilia wasilisho la taarifa katika kikao cha Sekretarieti ya Tume kilichofanyika tarehe 29 Septemba, 2026.