HISTORIA YA TUME
Tume ya Pamoja ya Fedha ni Asasi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoundwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 134 na kuanzishwa kupitia Sheria ya Tume ya Pamoja ya Fedha ya Mwaka 1996, Sura 140 Tume ya Pamoja ya Fedha inatekeleza majukumu yake chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, SMT.
Jukumu la msingi la Tume ni kushauri na kutoa mapendekezo kuhusu Uhusiano wa Kifedha baina ya SMT na SMZ Jukumu hili limeainishwa bayana katika Katiba kupitia Ibara 133 na 134.
Aidha, Katiba ya Zanzibar kupitia Ibara ya 124 inatambua mamlaka ya Tume ya Pamoja ya Fedha kutekeleza majukumu yake Zanzibar. Tume ilianza kutekeleza rasmi majukumu mwaka 2003.
Hadi sasa, Tume imetoa Ushauri na Mapendekezo kuhusu masuala mbalimbali ya Uhusiano wa Kifedha na kuwasilisha kwa Serikali zote mbili. Ushauri na Mapendekezo hayo yamegawanyika katika maeneo ya: Usimamizi wa Mapato ya Muungano; Usimamizi wa Matumizi ya Muungano; Ukopaji nje ya Nchi; na Uhaulishaji wa fedha kati ya Serikali mbili. Baadhi ya mapendekezo hayo yametekelezwa kikamilifu. Aidha mapendekezo mengine , Serikali mbili zinaendelea na majadiliano na mashauriano kwa ajili ya kufikia uamuzi.
Katika kusimamia na kutekeleza majukumu ya Tume, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Ibara 134(1) ya Katiba amepewa mamlaka ya kuteua Makamishna wa Tume wasiozidi saba, ambao hutekeleza majukumu yao kwa kipindi cha miaka mitano .Aidha, sheria imeruhusu makamishna hao kuteuliwa tena kwa kipindi kingine kisichozidi miaka mitano. . Hadi sasa, Rais ameteua awamu tatu za Makamishna wa Tume kama ifuatavyo:
Makamishna katika Kipindi cha Kwanza (2003 hadi 2008)
- Mhe. William H. Shellukindo (Mb) Mwenyekiti
- Bw. Khamis M. Omar Makamu Mwenyekiti
- Balozi Charles M. Nyirabu[1] Kamishna
- Dkt. Edmund B. Mndolwa Kamishna
- Dkt. Hawa Sinare Kamishna
- Bi Amina Zidikheri Kamishna
- Bw. Simai P. Makame[2] Kamishna
Makamishna katika Kipindi cha Pili (2008 hadi 2013)
- Bw. William H. Shellukindo Mwenyekiti
- Bw. Abdulrahman M. Jumbe Makamu Mwenyekiti
- Bw. Khamis M. Omar Kamishna
- Mhe. Othman M. Othman (MBLW) Kamishna
- Dkt. Edmund B. Mndolwa Kamishna
- Dkt. Alhj. Juma Ngasongwa Kamishna
- Mhe. Dkt. Pindi H. Chana (Mb) Kamishna
Makamishna katika Kipindi cha Tatu (2014 – 2019)
- Bw. Abdulrahman M. Jumbe Mwenyekiti.
- Alhaj Dkt. Juma Ngasongwa Makamu Mwenyekiti.
- Bw. Othman M. Othman Kamishna
- Bw. Juma A. Hafidh Kamishna
- Bi. Edna N. Nyanguli Kamishna
- Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (MB) Kamishna
- Alhaj. Ramadhani M. Khijjah Kamishna
[1] Dk. Idris M. Rashid aliteuliwa Mei, 2006 kujaza nafasi ya Balozi Charles M. Nyirabu aliyefariki dunia.
[2] Bw. Taymour S. Juma aliteuliwa Februari, 2005 kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Simai P. Makame aliyefariki dunia.