KUANZISHWA
KUANZISHWA
Tume ya Pamoja ya Fedha ni Taasisi ya Serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoundwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 134 na ilianzishwa kupitia Sheria ya Tume ya Pamoja ya Fedha, Sura 140.
Jukumu la Msingi la kuanzishwa Tume ni kutoa Ushauri na Mapendekezo kuhusu masuala yanayohusu Uhusiano wa Kifedha kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Tume ilianza kutekeleza majukumu yake mwaka 2003.