Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Fedha

Tume ya Pamoja ya Fedha

JFC Logo
ZIARA YA MENEJIMENTI YA TUME KUKAGUA UKARABATI WA JENGO LA OFISI ZA TUME, LILILOPO KIVUKONI, DAR ES SALAAM
01 Jun, 2026
ZIARA YA MENEJIMENTI YA TUME KUKAGUA UKARABATI WA JENGO LA OFISI ZA TUME, LILILOPO KIVUKONI, DAR ES SALAAM

Menejimenti ya Tume ya Pamoja ya Fedha ikiongozwa na Katibu wa Tume, Bw. Ernest Mchanga, tarehe 28 Mei, 2026 imefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa jengo la Ofisi za Tume unaoendelea katika eneo la Kivukoni, Dar es Salaam. Ziara hiyo ililenga kuona hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa ukarabati huo.

Jengo hilo linatarajiwa kuwa makao mapya ya Tume ya Pamoja ya Fedha baada ya kuhama kutoka Ofisi zake za sasa zilizopo katika Jengo la Sukari, Posta, Dar es Salaam.