Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Fedha

Tume ya Pamoja ya Fedha

JFC Logo
JFC YAWAJENGEA UELEWA WATUMISHI WAKE KATIKA ENEO LA UHUSIANO WA KIFEDHA
19 Jul, 2024
JFC YAWAJENGEA UELEWA WATUMISHI WAKE KATIKA ENEO LA UHUSIANO WA KIFEDHA

Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha, Bw.Ernest Maduhu Mchanga (wa tano kulia) katika picha ya pamoja na watumishi wa Tume baada ya Semina ya kuwajengea uelewa kuhusu Uhusiano wa Kifedha kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Giraffe, Dar es salaam, tarehe 18, Julai 2024.

 

Tume ya Pamoja ya Fedha ilifanya semina yenye lengo la kuwajengea uelewa watumishi wake kuhusu Uhusiano wa Kifedha kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Semina hiyo ya siku moja ilifanyika tarehe 18 Julai katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Girrafe iliyopo Mbezi, Dar es salaam.

Awali akifungua semina hiyo, Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha, Bw. Ernest Maduhu Mchanga alieleza kuwa, “semina hii imeandaliwa ili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu Uhusiano wa Kifedha na  majukumu ya Tume. Tunapotoka hapa kila mmoja aweze kuelewa Tume ilianzishwa lini, muundo wake na akaunti ya fedha ya pamoja.

Bw. Mchanga alifafanua pia kuwa, semina hiyo ni fursa kwa watumishi wote kupata uelewa wa kutosha kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Tume.