JFC YASHIRIKI MAONESHO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO – ZANZIBAR

Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, mkewe Mama Mariam Mwinyi na Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, wakimsikiliza Katibu Msaidizi wa Tume ya Pamoja ya Fedha Bw. Jonas Hungwi Nduttu akitoa maelezo kwa ufupi kuhusu majukumu ya Tume, alipotembelea banda la Tume siku ya ufunguzi wa Maonesho ya Muungano katika viwanja vya Nyamanzi – Zanzibar.
Tume ya Pamoja ya Fedha ilishiriki maonesho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika katika viwanja vya Nyamanzi- Zanzibar kuanzia tarehe 14 Aprili hadi tarehe 20 Aprili, 2024. Uzinduzi wa maonesho hayo ulifanyika tarehe 14 Aprili, mgeni rasmi akiwa Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Mhe. Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi alitembelea banda la Tume na kupata maelezo kwa ufupi kuhusu majukumu ya Tume kutoka kwa Katibu Msaidizi Bw. Jonas Hungwi Nduttu.
Mwanachi akipata elimu kutoka kwa Afisa wa Tume, Bi. Gugwa Juma Barisiba alipotembelea banda la Tume katika viwanja vya Nyamanzi – Zanzibar
Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha Bw. Ernest Maduhu Mchanga (katikati) katika picha ya pamoja na Katibu Msaidizi Bw. Jonas Hungwi Nduttu (kulia), CPA. Rehema Ephron Mwakajube – Mhasibu Mkuu na Watumishi wa Tume ya Pamoja ya Fedha baada ya Ufunguzi wa maonesho ya miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Nyamanzi- Zanzibar.
Aidha, Tume ya Pamoja ya Fedha ilishiriki maonesho ya Muungano yaliyofanyika Tanzania Bara katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es salaam kuanzia tarehe 19 hadi tarehe 25 Aprili, kisha kuhudhuria kilele cha Maadhimisho ya siku ya Muungano tarehe 26 Aprili, 2024 katika Uwanja wa Uhuru – Dar es salaam. Mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo alikuwa ni Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .