Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Fedha

Tume ya Pamoja ya Fedha

JFC Logo
JFC YAMUAGA MWENYEKITI WA SEKRETARIETI YA TUME BW. AHMED SAADAT
25 Oct, 2024
JFC YAMUAGA MWENYEKITI WA SEKRETARIETI YA TUME BW. AHMED SAADAT

Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha Bw. Ernest M. Mchanga (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Tume Bw. Ahmed H. Saadat (kushoto), zawadi ya saa yenye ujumbe maalum wa shukrani, katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika tarehe 24 Oktoba, 2024.


Wajumbe wa Sekretarieti, Menejimenti na Watumishi wa Tume ya Pamoja ya Fedha walifanya hafla fupi ya kumuaga Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Tume Bw. Ahmed H. Saadat anayetarajia kustaafu ifikapo tarehe 30 Oktoba, 2024.


Hafla hiyo ilifanyika tarehe 24 Oktoba, 2024 muda mfupi baada ya kuhitimisha  Kikao cha Sekretarieti ya Tume ya Pamoja ya Fedha.


Akitoa salamu za shukrani, Bw. Saadat amewashukuru Wajumbe wa Sekretarieti, Menejimenti na Watumishi wa Tume kwa ushirikiano wao katika kipindi chote alichofanya nao kazi. Aidha, amebainisha kuwa Tume ni chombo muhimu katika kutoa Ushauri kuhusu Uhusiano wa Kifedha kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, hivyo kuwa sehemu ya Tume ni nafasi adhimu.


Kwa upande wake, Katibu wa Tume kwa niaba ya Menejimenti amemshukuru Bw. Saadat kwa mchango alioutoa akiwa Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Tume katika kipindi cha miaka sita ya uongozi wake.


Aidha, kwa niaba ya Wajumbe wa Sekretarieti na Watumishi amemkabidhi zawadi na kumtakia kheri katika safari mpya ya maisha ya kustaafu.


Bw. Ahmed Saadat amekuwa Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Tume ya Pamoja ya Fedha kwa muda wa miaka sita kuanzia mwaka 2018 hadi 2024, akimwakilisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar.