Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Fedha

Tume ya Pamoja ya Fedha

JFC Logo
SEKRETARIETI YA TUME YAFANYA KIKAO CHA TATU KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24
28 May, 2024
SEKRETARIETI YA TUME YAFANYA KIKAO CHA TATU KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24

Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Tume ya Pamoja ya Fedha, Bw. Ahmed H. Saadat (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti, na Makatibu Wasaidizi, Bi. Agnes J. Bhwana (wakwanza kushoto) Kaimu Katibu Msaidizi-Idara ya Huduma Saidizi na Bw. Jonas H. Nduttu (wapili kulia) Katibu Msaidizi – Idara ya Huduma za Kiufundi, baada ya kikao cha Sekretarieti ya Tume kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Giraffe, Dar es salaam, tarehe 23 na 24, Mei 2024.

Wajumbe wa Sekretarieti katika Picha.

Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Tume ya Pamoja ya Fedha, Bw. Ahmed H. Saadat (wanne kushoto) kutoka Mamlaka ya Mapato Zanzibar; Bw. Ernest M. Mchanga (watatu kushoto), Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha; Bi. Hanifa M. Selengu (wapili kushoto) kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Bw. Ali A. Hassan (wakwanza kulia)kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Zanzibar; Bi. Sia A. Shayo (wanne kulia) kutoka Benki Kuu ya Tanzania na Bi. Yosepha A. Tamamu (watatu kulia) kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania.

 

Sekretarieti ya Tume ya Pamoja ya Fedha imefanya kikao cha tatu kwa Mwaka wa Fedha 2023/24. Kwa mujibu wa Sheria ya Tume ya Pamoja ya Fedha ya mwaka 1996 Sura 140, Kifungu 11(1), inataja Sekretarieti ya Tume kuwa ni Chombo tendaji chenye wajibu wa kuchambua na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Makamishina kuhusu masuala mbalimbali ya Uhusiano wa Kifedha baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).