Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Fedha

Tume ya Pamoja ya Fedha

JFC Logo
KAMATI YA BAJETI YA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR YAFANYA ZIARA JFC
22 May, 2024
KAMATI YA BAJETI YA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR YAFANYA ZIARA JFC

Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Mwanaasha Khamis Juma akisaini daftari la wageni, alipofanya ziara Tume ya Pamoja ya Fedha – Dar es salaam.

Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar imefanya ziara katika Ofisi ya Tume ya Pamoja ya Fedha – Dar es salaam siku ya Jumatatu tarehe 15 Aprili, 2024 kwa lengo la kujifunza na kuona utekelezaji wa majukumu ya Tume.

Ziara hiyo ya siku moja iliongozwa na Mhe. Mwanaasha Khamis Juma ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, akiambatana na Makamo Mwenyekiti Mhe. Dkt Soud Nahoda Hassan na  wajumbe wengine sita, ambao ni Mhe. Asha Abdalla Mussa, Mhe. Mohamed Mgaza Jecha, Mhe. Prof. Omar Fakih Hamad, Mhe. Rukia Omar Ramadhan, Mhe. Yussuf Hassan Iddi na Mhe. Suleiman Masoud Makame.

Aidha, Mhe. Mwanaasha Khamis Juma aliongozana na Makatibu wa Kamati Ndg. Asha Said Mohamed, Ndg. Husna Rajab Othman, Ndg. Shaib Fadhil Shaib na Maafisa uratibu, Bi. Hafssa Omar Khamis na Bi. Maryam Ali Juma.

Mhe. Mwanaasha Khamis Juma kwa niaba ya Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, alihitimisha ziara hiyo kwa kuishukuru Tume kwa mapokezi mazuri na kuhimiza kudumisha ushirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kifedha. Sanjari na hayo alitoa pongezi kwa hatua nzuri ya utekelezaji wa majukumu ya Tume.