Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Fedha

Tume ya Pamoja ya Fedha

JFC Logo
JFC YASHIRIKI MAONESHO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO, MNAZI MMOJA, DAR ES SALAAM.
22 May, 2024
JFC YASHIRIKI MAONESHO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO, MNAZI MMOJA, DAR ES SALAAM.

Afisa wa Tume ya Pamoja ya Fedha Bw. George Lucas Maige, akitoa elimu kwa Mwananchi aliyetembelea banda la Tume katika maonesho ya Taasisi za Muungano yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es salaam kuanzia tarehe 19 hadi 25 Aprili, 2024.

Tume ya Pamoja ya Fedha ni miongoni mwa Taasisi za  Muungano zilizoshiriki Maonesho ya miaka 60 ya Muungano yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es salaam kuanzia tarehe 19 Aprili hadi 25 Aprili, 2024.

Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi na Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, tarehe 19 Aprili, 2024.

Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha Bw. Ernest Maduhu Mchanga ( watatu kulia), Kaimu Katibu Msaidizi Bi. Agnes Joseph Bhwana ( watatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Tume siku ya ufunguzi wa maonesho ya Taasisi za Muungano, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

 

Watumishi wa Tume wakiwa tayari kuwahudumia Wananchi wanaotembelea banda la Tume ya Pamoja ya Fedha katika maonesho ya Miaka 60 ya Muungano, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es salaam kuanzia tarehe 19 hadi 25 Aprili, 2024.

Aidha, Tume ilishiriki kilele cha maadhimisho ya siku ya Muungano tarehe 26 Aprili, 2024 katika Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam. Mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan. Maadhimisho hayo yalikuwa na Kauli Mbiu isemayo, "Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Tumeshikamana na Tumeimarika kwa Maendeleo ya Taifa Letu'.