Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Fedha

Tume ya Pamoja ya Fedha

JFC Logo
BW. AHMED SAADAT AREJEA KUENDELEA NA NAFASI YA UENYEKITI WA SEKRETARIETI YA TUME YA PAMOJA YA FEDHA
20 Mar, 2025
BW. AHMED SAADAT AREJEA KUENDELEA NA NAFASI YA UENYEKITI WA SEKRETARIETI YA TUME YA PAMOJA YA FEDHA

Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha Bw. Ernest Mchanga (wa tatu kulia) pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Tume wakimkaribisha Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Tume, Bw. Ahmed Saadat (wa tatu kushoto) baada ya kuongezwa muda wa utumishi wa umma, hivyo kuendelea kumwakilisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar katika nafasi ya Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Tume ya Pamoja ya Fedha.

 

Wajumbe wa Sekretarieti, Menejimenti na Watumishi wa Tume ya Pamoja ya Fedha, katika kikao cha Sekretarieti kilichofanyika tarehe 24 Oktoba, 2024 walimuaga Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Tume Bw. Ahmed H. Saadat aliyekuwa anatarajia kustaafu utumishi wa umma ifikapo tarehe 30 Oktoba, 2024.

Kufuatia kuongezewa muda wa utumishi wa umma na Mwajiri wake, Bw. Saadat amerejea kumwakilisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar katika nafasi ya Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Tume ya Pamoja ya Fedha, kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Akizungumza katika kikao cha Sekretarieti kilichofanyika tarehe 12 Machi, 2025, Bw. Ahmed Saadat alishukuru kupata nafasi ya kuendelea kumwakilisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Katibu wa Tume, Bw. Ernest Mchanga kwa niaba ya Wajumbe wa Sekretarieti na Watumishi alimkaribia Mwenyekiti wa Sekretarieti na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya Sekretarieti ya Tume.